×

Eneo la Simba wala watu wa Tsavo

Wafanya kazi waliokuwa wakijenga reli katika enzi za ukoloni. [File, Pambazuko]

Mbuga ya kitaifa ya hifadhi ya Tsavo ndio kubwa zaidi nchini na ya pili kwa ukubwa duniani baada ya ile ya kitaifa ya Kruger iliyoka Afrika Kusini, ikiwa na ukubwa wa kilomita 21,000 mraba. Mbuga hii ambayo imegawanywa sehemu mbili ya Tsavo Mashariki na Magharibi ina sifa kemkem duniani kama hifadhi ya wanyama maarufu watano yaani Big Five ambao ni chui, ndovu, kifaru, simba na nyati. Hata hivyo simba wa mbuga ya Tsavo wanaotofauti na wale wengine ulimwenguni  kwani wale wa kiume hawana nywele nyingi kichwani , hivyo kuwa vigumu kidogo kuwatofautisha na wale wa kike.

 Fauku ya hayo simba wa Tsavo wana historia kabambe hasa wale simba wala watu wawili alimaarufu kama Man Eaters of Tsavo. Simba hawa ndio kiini cha jina la eneo liitawalo Man Eaters lililoko kwenye barabara kuu ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi, yapata  kilomita 40 kutoka mji wa Voi.

 Eneo hili lina mvuto sana kimaumbile na kipenzi cha watalii kutoka nje mwa nchi na pia wageni wa humu nchini. Hoteli ya  kitalii ya Man Eaters ni mojawapo ya rasilimali za kitalii mbapo wageni kwenye mbuga ya Tsavo huenda kujivinjari. Hata hivyo wageni wengi kwenye eno hili yamkini hawafahamu historia iliyochangia eneo hilo kupewa jina la Man Eaters.

Kuna wale wanahisi kuwa eneo hilo linaandamwa  na mikosi au  laana fulani kutokana na jinamizi la ajali za magari zinazotokea mara kwa mara kwenye eneo hilo ambapo mamia ya abiria huaga dunia na mamia wengine kujeruhiwa vibaya. Aliyekuwa kwa wakati mmoja  mbunge wa Voi na mwimbaji hodari wakati wa enzi ya serikali ya Kanu marehemu Boniface Mghanga aliaga dunia kwenye ajali mbaya eneo la Man Eaters miaka michache iliyopita. Msomi mtajika kutoka Pwani ambaye pia alikuwa mwanama.

 “Mwili wa mmoja wa mashahidi kwenye kesi iliyokuwa inawakabili Uhuru Kenyatta na William Ruto kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) pia ulipatikana umetupwa kwenye eneo la Man Eaters baada ya kuripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana.”

“Ni eneo lenye historia yakusisimua na pia mahali ambapo miili ya wafu hutupwa ili ziliwe na wanyamapori na hivyo kuharibu.”

Barabara ya reli kutoka Mombasa mnamo 1900 ni wakati huu ambapo wengi waliliwa na simba hapa.geuzi wakati kwa serikali ya Nyayo Profesa Katama Mkangi  pia aliaga dunia kwenye ajali eneo hilo. Kwa upande mwingine, mwili wa msomi mtatanishi wa dini ya Kiislamu Sheikh Samir Khan, ambaye hapo awali aliripotiwa kupotea, ulipatikana umetupwa kwenye eneo hilo na watu wasiojulikana. Mwili wa mmoja wa mashahidi kwenye kesi iliyokuwa inawakabili Uhuru Kenyatta na William Ruto kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) pia ulipatikana umetupwa kwenye eneo la Man Eaters baada ya kuripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana.

 Miili hii yamkini hutupwa kwenye eneo hili ili iliwe na wanyamapori na hivyo kuharibu ushahidi juu ya mauaji hayo. Historia ilionekana kujirudia wakati wa ujenzi wa reli ya kisasa alimaarufu SGR ambapo ripoti ambazo hazikudhibitishwa zilidai wafanyi kazi walishambuliwa na chui na simba wakati wa harakati zao. Ingawa ajali nyingi kwenye eneo la Man Eaters zinadaiwa kuchangiwa na uendashaji mbaya wa magari na makosa ya kibinadamu kuna wale wana maono tofauti. Kuna madai kwamba eneo hilo ni baadhi ya sehemu zijulikanazo kama fi ghi kwenye mila ya Kitaita.

Fighi ni tambiko za kimila ambazo zilikuwa zinafanywa wakati wa miaka ya zamani ili kukinga eneo la Taita kuvamiwa na watu kutoka nje. “Kimila, fighi ni tambiko za madawa ya kiasili ambazo wazee wateule na waganga walikuwa wakifanya kwenye mipaka ya Taita na majirani zao ili kuzuia eneo hilo kuingiliwa na watu wabaya.

“Watu hao wachokozi wanadaiwa kukumbana na hali tata kama vile kuumwa na nyuki au kushambuliwa na wanyama wakali punde tu walipojaribu kuingia kwenye eneo lililomilikiwa wa na wataita” asema mzee Ronald Mwangura wa miaka 67. Mzee Mwangura anadai kwamba wazee wakitaita walikuwa wakitoa kafara mara kwa mara kwenye sehemu za fi ghi ili kuzipatia nguvu na pia kufurahisha mizimu ya wazee wa kitaita ili mikosi isikumbe jamii hiyo.

 Mwangura anasema kwamba kupuuzwa kwa mila na desturi za kiasili baada wa dini ya Kikiristo kuwasili kutoka ng’ambo ni mojawapo ya sababu ya ajali mbaya na mikosi inayokumba eneo la Man Eaters kwani mizimu ya wazee wa kale wa Kitaita wamekerwa na kukasirika kwa sababu ya kutelekezwa.

 “Kuna sehemu nyingi za fi ghi Taita mojawapo ikiwa karibu na sehemu ya Maungu karibu na mji wa Voi, pale Josa karibu na mji wa Wundanyi na sehemu ya Mariwenyi. Ni sadfa  kwamba sehemu hizi hutokea ajali mbaya mara kwa mara,” asema mzee Mwangura. Wakwasi wa maswala ya mila na desturi wanadai kwamba Simba wawili wala watu  hawakuwa simba wa kawaida bali mizimu iliyotabiriwa na wazee kama Mwakishaluwa ili kuzuia reli ama“Nyoka ya chuma” kupitia eneo la Taita bila wazee watajika kutoka Taita kuhusishwa kikamilifu. Inadaiwa kwamba Mwakishaluwa alikuwa na ndumba kali za kimadawa na mizimu mojawapo ikiwa ile ya kuwatumia mahasimu wake wanyamapori hatari ili kuwaumiza au kuwaharibia mimea na mali.

Baada ya kukamilisha waliyotumwa kufanya wanyama hao wangerudi tena mbugani Tsavo. Simba wala watu hao  wawili walioitwa majina “Ghost” na “ Darkness” wamenakiliwa kwenye sinema maarufu ulimwenguni ijulikanayo kama “ The Ghost and The darkness” . Simba hao wanadaiwa kuwageuza kitoweo wajenzi wa reli ama  “coolies” 130 kwenye kivuko cha mto Tsavo. Kisanga hiki kilitokea mwaka 1898 wakati wabeberu wakijenga reli kutoka Mombasa kuelekea Kisumu wakiongozwa na Luft ena Kanali John Henry Patterson. Inadaiwa licha ya wajenzi wa reli kuwasha moto kuwatisha simba hao wawili, waliruka juu ya moto huo na kuwakamata wafanyi kazi hao kisha kuwala.

 Patterson anadaiwa kujaribu kuweka mitego tofauti tofauti ili kuwanasa simba hao na baada ya vita vikali Patterson alimpiga risasi na kumuua simba wa kwana mnamo tarehe 9 Desemba mwaka 1898. Siku ishirini baadaye Luft ena Kanali Patterson alimwangamiza simba wa pili kwa kumpiga risasi.

 Yasemekana kwamba Patterson alichuna ngozi ya simba hao na kuitumia kama zulia kwa miaka 25 na kisha kuuza mabaki ya wanyama hao kwa dola za Marekani 5,000 kwenye Chicago Field Museum ya Marekani ambapo hali waleo bado ni kivutio kikubwa kwa wageni na watalii. Kuna baadhi ya wakenya ambao wamekuwa wakiomba mabaki ya simba hao maarufu yarudishwe nchini kutoka Marekani na kuhifadhiwa kwenye makafadhi ya kitaifa ya Kenya kama mojawapo ya turathi na kiungo.